Jumapili 16 Agosti 2026 - 13:45
Muqawama Unaelekea Kwenye Chaguo Zake, Na Yeyote Anayetegemea Kujisalimisha Ameegemea Kwenye Sarabi (Mazigazi)

Hawza/ Katibu Mkuu wa Hizbullah, Sheikh Naim Qassem, katika maadhimisho ya miaka 20 ya ushindi katika Vita vya Siku 33, huku akisisitiza kwamba Muqawama una uwezo wa kubadilisha mlingano wa nguvu, alisema: “Dunia nzima ilishuhudia ushindi wa Julai 2006.”

Kwa mujibu wa Idara ya tarjama ya Shirika la Habari la Hawza, Sheikh Naim Qassem, Katibu Mkuu wa Hizbullah, katika maadhimisho ya miaka 20 ya ushindi wa Vita vya Siku 33 vya Julai 2006 (1385 Hijria ya Shamsia), akisisitiza kwamba Muqawama una uwezo wa kubadilisha mlingano wa nguvu, alisema: Dunia nzima ilishuhudia ushindi wa Julai 2006, na huu ni mfano unaoonyesha kwamba Muqawama una uwezo wa kubadilisha mlingano wa nguvu; na huu ni uzoefu uliopo na unaoendelea. Ndiyo, jambo hili linahitaji maandalizi na utafiti wa hali halisi, lakini hili ni miongoni mwa uzoefu ulio mbele yetu.

Alirejea Vita vya Julai 2006, vilivyomalizika kwa kushindwa adui wa Israel, na kusema: Adui huyu mwenye kiburi, huku Marekani ikiwa nyuma yake, walikabiliana na Muqawama wa Kiislamu nchini Lebanon pamoja na wapiganaji wote wenye heshima katika mfumo wa jeshi, taifa na Muqawama. Miongoni mwa matokeo ya operesheni hiyo ilikuwa ni kuachiwa huru  wafungwa na mahabusu waliokuwa mikononi mwa watekaji.

Sheikh Qassem alisema: Mpango wa wakati huo ulikuwa mkubwa — yaani, mpango wa “Mashariki ya Kati Mpya” — lakini ulishindwa na kutoweka, huku kinga ya kuzuia mashambulizi dhidi ya adui ikiendelea kuwepo kuanzia mwaka 2006 hadi 2023 (1385 hadi 1402 Hijria ya Shamsia).

Katibu Mkuu wa Hizbullah alieleza: Adui alisalimu amri mbele ya Muqawama huu, taifa hili na Lebanon yenye msimamo na inayopinga uvamizi. Miongoni mwa matokeo yake ni kwamba; kinga ya kuzuia mashambulizi dhidi ya adui wa Israel iliendelea kuwepo kuanzia mwaka 2006 hadi 2023. Hii ni dalili ya umuhimu wa Muqawama na ni mfano unaothibitisha kwamba Muqawama una uwezo wa kubadilisha mlingano wa nguvu; na huu ni uzoefu uliopo na unaoendelea.

Kuhusu maendeleo ya sasa alisema: “Miongoni mwa matokeo ya vita vya ‘Awli al-Ba’s’ (Shambulio la Kwanza) ni makubaliano ya Oktoba 2024, ambayo yanataka adui aondoke.” Alieleza kwamba; makubaliano hayo bado yanaendelea kuwa na uhalali na ndiyo yanayoweka kiwango cha juu cha hatua zetu, hata hivyo viongozi wa Lebanon hawakuona chochote isipokuwa silaha ya Muqawama na wakaanza kuilenga; hawakushirikiana, bali walikuwa chini ya udhamini ambao matokeo ya hatua zao yameuweka wazi.

Aliongeza kusema: Muqawama ulimzuia adui kufikia malengo yake na unaendelea kuwa thabiti katika kufuata chaguo zake, na yeyote anayetegea kujisalimisha, ameshikilia sarabi na haujui Muqawama ipasavyo. Muqawama na watu wake umevumilia na kuwa na subira, kwa sababu unakabiliwa na chaguo ambazo, iwapo zitasababisha kujisalimisha na kuanguka, hazikubaliki.

Sheikh Naim Qassem, akieleza kwamba kama vita visingeanza tarehe 2 Machi (12 Esfand 1402 Hijria ya Shamsia), vingekuwa vimeanza baadaye, alisisitiza: Hivi vilikuwa vita vya uchokozi na vya kuweka uwepo, ambavyo Muqawama ulivijibu kwa mapambano ya mtindo wa Karbala.

Kuhusu kile kinachoitwa “Makubaliano ya Mfumo”

Katibu Mkuu wa Hizbullah aliyataja makubaliano hayo kuwa ni maagizo ya Israel yenye wino wa Israel, ambayo viongozi wa Lebanon wanayatia saini chini ya usimamizi na ushiriki wa Marekani, huku tatizo kuu likiwa katika mazungumzo ya moja kwa moja na maudhui yake yote kuanzia mwanzo hadi mwisho.

Sheikh Qassem alisema: Wote waliotazama tukio hilo kutoka Washington waliona timu moja iliyokuwa ikiitwa timu ya Marekani na Israel, lakini timu ya Lebanon ilikuwa tegemezi na ilitekeleza yale yaliyokuwa yakisemwa na Marekani.

Sheikh Qassem aliwaambia viongozi: “Tuonesheni fanikio hata moja lililopatikana katika raundi saba za mazungumzo; kila kitu adui wa Israel amekipata na kila anachokitaka.”

Akieleza kushangazwa kwake na hatua za viongozi, aliuliza: “Ni ubunifu gani huu ambao mmeuita maeneo ya majaribio? Na mnawezaje, badala ya kulitetea jeshi, kukubali kulidhalilisha? Je, Zoutar al-Gharbi haijakaliwa kimabavu, bali ni eneo la majaribio mpaka Israel iwape ruhusa ya kuingia?”

Alisisitiza: “Makubaliano ya Mfumo” yaliwanyima viongozi uwezo wa kumfuatilia adui kisheria katika mahakama na yalisababisha kukaliwa kwa al-Mansouri, Zoutar al-Gharbi, al-Ghaziya na al-Aar.

Katibu Mkuu wa Hizbullah aliwataka viongozi wa Lebanon kurejea nyuma kutoka katika kosa hilo na kurejea kwa watu wao, pamoja na kutumia vipengele vya nguvu. Alieleza kushangazwa na kutowajibu kwao Katz na Netanyahu, huku akisisitiza: Kinachotokea ni kujisalimisha, na sisi hatukikubali wala hatutakubali Marekani iamue na kuiiba nchi na mustakabali wake.

Sheikh Qassem alisisitiza: Leo, kusini inapaswa kuwa suala la msingi; wakimbizi wanapaswa kushughulikiwa, na lazima kuwepo makazi, misaada na ukarabati wa uharibifu. Serikali ndiyo yenye jukumu kubwa kuliko taasisi nyingine yoyote, ni kweli kwamba sisi tumekuwa mstari wa mbele katika kutoa msaada, ushirikiano na kufanya kila juhudi kadiri iwezekanavyo, lakini msingi ni kwamba serikali itekeleze wajibu wake, na sisi tutaendelea kufuatilia kufanikisha jambo hilo.

Sheikh Qassem aliwaambia wananchi wenye heshima: Kila neno tunalolisema mbele ya yale mliyoyafsnya katika kujitolea na kutoa mhanga, ni jambo dogo sana. Tunawaona kuwa wakubwa, ninyi ni taji la vichwa vyetu, na tunawaambia kwamba tutatoa maisha yetu kwa ajili yenu na tutapigana hadi tone la mwisho la damu, sisi sote tuko pamoja katika ngome moja.

Aliongeza kusema: Mna haki ya kukasirika na kuonyesha hasira zenu, lakini tunawaomba muihifadhi hasira hiyo ndani yenu na kuiandaa kwa ajili ya kutumika wakati mwafaka, ili kufanikisha malengo na matakwa yenu.

Sheikh Naim Qassem aliendelea kusema: Hasira pia ina wakati wake maalumu na huenda ikalipuka. Lakini mlipuko huo utakuwa wa namna gani? Kwa hiyo, wale ambao hawajui njia sahihi ya kushughulikia mambo na wanajaribu kuchukua hatua dhidi ya Muqawama na watu wa Muqawama, wanapaswa kubeba jukumu la madhara yatakayotokana na hilo.

Alieleza kuws: Jukumu la madhara hayo watalibeba wale wanaouvamia Muqawama, watu wa Muqawama, Lebanon, mustakabali wa Lebanon na mamlaka ya Lebanon.

Sheikh Qassem aliwaambia wapiganaji wenye heshima kwa kusema: Enyi mataji ya vichwa, enyi alama za heshima na mifano ya kujitolea, na enyi nuru za uhuru na kujitegemea; ninyi mmefanikiwa duniani na Akhera, na tunajivunia kuwa pamoja nanyi katika mapambano ya uhuru, heshima na utu wa mwanadamu.

Sheikh Qassem aliwashukuru wote wanaoshiriki, kutoka katika vyama, makundi na madhehebu mbalimbali, katika harakati zote zinazopinga ukaliaji wa ardhi kwa mabavu, kukabiliana na uchokozi, na kupinga makubaliano ya udhalilishaji na kuanzishwa kwa uhusiano wa kawaida.

Pia aliisifu roho ya mshikamano wa kijamii na kubainisha: Tumeungana sote kwa ajili ya kuondoa mateso katika nyanja za elimu, jamii, makazi na hali ya kiuchumi. Mshikamano huu wa kijamii ni muhimu sana katika kuziba mapengo yaliyoachwa na serikali hii kutokana na kutofanya kazi kwa umakini na kwa ufanisi katika mwelekeo chanya.

Sheikh Qassem aliendelea: Tuna deni kwa mashahidi wetu watukufu ambao wametutangulia kuelekea kwenye Arshi na kutengeneza njia kuelekea mustakabali bora. Mashahidi wetu wametuachia amana ambayo tutailinda na tutaendelea imara katika njia yao. Mashahidi wetu, katika kiwango cha Lebanon, katika suala la Palestina na katika ngazi ya dunia nzima, ni alama na mfano wenye heshima na wa kujivunia, kwa sababu wao ni mfano wa kujitolea na ukarimu.

Sheikh Qassem aliwaambia waliojeruhiwa: Mwenyezi Mungu awape heshima na awainue kwa ajili ya kujitolea huku kukubwa mliyokufanya katika njia hii adhimu.

Katibu Mkuu wa Hizbullah alisema: Hatutawaacha wafungwa wetu; tutaendelea na madai, juhudi na shughuli zetu za kuwaweka huru — Inshaallah.

Alisema mwishoni: Inshaallah, vipindi vya ushindi viko mbele yetu, na licha ya maumivu yote, tunapaswa kuvumilia; kwa sababu tumesimama imara, na kusimama kwetu imara kutakuwa miongoni mwa vituo vya ushindi.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha